Isaya 43:25
Isaiah 43:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako, kwa ajili yangu mwenyewe, wala sizikumbuki dhambi zako tena.
Isaiah 43:25 in English
Isaiah 43:25 · Berean Standard Bible
I, yes I, am He who blots out your transgressions for My own sake and remembers your sins no more.
Context
23Hujaniletea kondoo kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa,
wala kuniheshimu kwa dhabihu zako.
Sikukulemea kwa sadaka za nafaka
wala kukuchosha kwa kuhitaji uvumba. 24Hukuninunulia uvumba wowote wenye manukato,
wala hukunipa kwa ukarimu
mafuta ya wanyama wa dhabihu zako.
Lakini umenilemea kwa dhambi zako,
na kunitaabisha kwa makosa yako. 25“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako,
kwa ajili yangu mwenyewe,
wala sizikumbuki dhambi zako tena. 26Tafakari mambo yaliyopita,
njoo na tuhojiane,
leta shauri lako uweze kupewa haki yako. 27Baba yako wa kwanza alitenda dhambi,
wasemaji wako wameasi dhidi yangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.