Isaya 42:7
Isaiah 42:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
kuwafungua macho wale wasioona, kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela, na kuwafungua kutoka gerezani wale wanaokaa gizani.
Isaiah 42:7 in English
Isaiah 42:7 · Berean Standard Bible
to open the eyes of the blind, to bring prisoners out of the dungeon and those sitting in darkness out from the prison house.
Context
5Hili ndilo asemalo Mungu, Bwana,
yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda,
aliyeitandaza dunia na vyote vitokavyo humo,
awapaye watu wake pumzi,
na uzima kwa wale waendao humo: 6“Mimi, Bwana, nimekuita katika haki;
nitakushika mkono wako.
Nitakulinda na kukufanya
kuwa Agano kwa ajili ya watu
na nuru kwa Mataifa, 7kuwafungua macho wale wasioona,
kuwaacha huru kutoka kifungoni waliofungwa jela,
na kuwafungua kutoka gerezani
wale wanaokaa gizani. 8“Mimi ndimi Bwana; hilo ndilo Jina langu!
Sitampa mwingine utukufu wangu
wala sanamu sifa zangu. 9Tazama, mambo ya kwanza yametokea,
nami natangaza mambo mapya;
kabla hayajatokea
nawatangazia habari zake.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.