Isaya 42:23
Isaiah 42:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili, au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao?
Isaiah 42:23 in English
Isaiah 42:23 · Berean Standard Bible
Who among you will pay attention to this? Who will listen and obey hereafter?
Context
21Ilimpendeza Bwana
kwa ajili ya haki yake
kufanya sheria yake kuwa kuu na tukufu. 22Lakini hili ni taifa lililoibwa na kutekwa nyara,
wote wamenaswa katika mashimo,
au wamefichwa katika magereza.
Wamekuwa nyara,
wala hapana yeyote awaokoaye.
Wamefanywa mateka,
wala hapana yeyote asemaye, “Warudishe.” 23Ni nani miongoni mwenu atakayesikiliza hili,
au atakayezingatia kwa makini katika wakati ujao? 24Ni nani aliyemtoa Yakobo kuwa mateka,
na Israeli kwa wateka nyara?
Je, hakuwa yeye, Bwana,
ambaye tumetenda dhambi dhidi yake?
Kwa kuwa hawakufuata njia zake,
hawakutii sheria zake. 25Hivyo akawamwagia hasira yake inayowaka,
ukali wa vita.
Iliwazunguka kwa miali ya moto, lakini hata hivyo hawakuelewa;
iliwateketeza, lakini hawakuyatia moyoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.