Isaya 41:8
Isaiah 41:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Lakini wewe, ee Israeli, mtumishi wangu, Yakobo, niliyemchagua, ninyi wazao wa Abrahamu rafiki yangu,
Isaiah 41:8 in English
Isaiah 41:8 · Berean Standard Bible
“But you, O Israel, My servant, Jacob, whom I have chosen, descendant of Abraham My friend—
Context
6kila mmoja humsaidia mwingine
na kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!” 7Fundi humtia moyo sonara,
yeye alainishaye kwa nyundo
humhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe,
Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.”
Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike. 8“Lakini wewe, ee Israeli, mtumishi wangu,
Yakobo, niliyemchagua,
ninyi wazao wa Abrahamu rafiki yangu, 9nilikuchukua toka miisho ya dunia,
nilikuita kutoka pembe zake za mbali.
Nilisema, ‘Wewe ni mtumishi wangu’;
nimekuchagua, wala sikukukataa. 10Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;
usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.
Nitakutia nguvu na kukusaidia;
nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.