Isaya 41:5
Isaiah 41:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Visiwa vimeliona na kuogopa, miisho ya dunia inatetemeka. Wanakaribia na kuja mbele,
Isaiah 41:5 in English
Isaiah 41:5 · Berean Standard Bible
The islands see and fear; the ends of the earth tremble. They approach and come forward.
Context
3Huwafuatia na kuendelea salama,
katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita. 4Ni nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza,
akiita vizazi tangu mwanzo?
Mimi, Bwana, ni wa kwanza
nami nitakuwa pamoja na wa mwisho:
mimi Bwana ndiye.” 5Visiwa vimeliona na kuogopa,
miisho ya dunia inatetemeka.
Wanakaribia na kuja mbele, 6kila mmoja humsaidia mwingine
na kusema kwa ndugu yake, “Uwe hodari!” 7Fundi humtia moyo sonara,
yeye alainishaye kwa nyundo
humhimiza yeye agongeaye kwenye fuawe,
Humwambia yeye aunganishaye, “Ni kazi njema.”
Naye huikaza sanamu kwa misumari ili isitikisike.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.