Isaya 41:3
Isaiah 41:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Huwafuatia na kuendelea salama, katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita.
Isaiah 41:3 in English
Isaiah 41:3 · Berean Standard Bible
He pursues them, going on safely, hardly touching the path with his feet.
Context
1“Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa!
Mataifa na wafanye upya nguvu zao!
Wao na wajitokeze, kisha waseme,
tukutane pamoja mahali pa hukumu. 2“Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki,
akimwita katika haki kwa utumishi wake?
Huyatia mataifa mikononi mwake,
na kuwatiisha wafalme mbele zake.
Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake,
huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake. 3Huwafuatia na kuendelea salama,
katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita. 4Ni nani aliyefanya jambo hili na kulitimiliza,
akiita vizazi tangu mwanzo?
Mimi, Bwana, ni wa kwanza
nami nitakuwa pamoja na wa mwisho:
mimi Bwana ndiye.” 5Visiwa vimeliona na kuogopa,
miisho ya dunia inatetemeka.
Wanakaribia na kuja mbele,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.