Native Bible

Isaiah 41:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa! Mataifa na wafanye upya nguvu zao! Wao na wajitokeze, kisha waseme, tukutane pamoja mahali pa hukumu.

Isaiah 41:1 in English

Isaiah 41:1 · Berean Standard Bible

“Be silent before Me, O islands,* and let the peoples renew their strength. Let them come forward and testify; let us together draw near for judgment.

Context

1“Nyamazeni kimya mbele zangu, enyi visiwa! Mataifa na wafanye upya nguvu zao! Wao na wajitokeze, kisha waseme, tukutane pamoja mahali pa hukumu. 2“Ni nani aliyemchochea mmoja kutoka mashariki, akimwita katika haki kwa utumishi wake? Huyatia mataifa mikononi mwake, na kuwatiisha wafalme mbele zake. Huwafanya kuwa mavumbi kwa upanga wake, huwafanya makapi yapeperushwayo na upepo kwa upinde wake. 3Huwafuatia na kuendelea salama, katika njia ambayo miguu yake haijawahi kupita.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.