Isaya 41:26
Isaiah 41:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua, au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’? Hakuna aliyenena hili, hakuna aliyetangulia kusema hili, hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu.
Isaiah 41:26 in English
Isaiah 41:26 · Berean Standard Bible
Who has declared this from the beginning, so that we may know, and from times past, so that we may say: ‘He was right’? No one announced it, no one foretold it, no one heard your words.
Context
24Lakini ninyi ni zaidi ya bure kabisa,
na kazi zenu hazifai kitu kabisa;
yeye awachaguaye ni chukizo sana. 25“Nimemchochea mtu mmoja kutoka kaskazini,
naye yuaja, mmoja toka mawio ya jua aliitaye Jina langu.
Huwakanyaga watawala kana kwamba ni matope,
kama mfinyanzi akanyagavyo udongo wa kufinyangia. 26Ni nani aliyenena hili tokea mwanzoni, ili tupate kujua,
au kabla, ili tuweze kusema, ‘Alikuwa sawa’?
Hakuna aliyenena hili,
hakuna aliyetangulia kusema hili,
hakuna yeyote aliyesikia maneno kutoka kwenu. 27Nilikuwa wa kwanza kumwambia Sayuni,
‘Tazama, wako hapa!’
Nilimpa Yerusalemu mjumbe wa habari njema. 28Ninatazama, lakini hakuna yeyote:
hakuna yeyote miongoni mwao awezaye kutoa shauri,
hakuna yeyote wa kutoa jibu wakati ninapowauliza.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.