Isaya 40:3
Isaiah 40:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sauti ya mtu aliaye: “Itengenezeni jangwani njia ya Bwana, nyoosheni njia kuu nyikani kwa ajili ya Mungu wetu.
Isaiah 40:3 in English
Isaiah 40:3 · Berean Standard Bible
A voice of one calling: “Prepare the way for the LORD in the wilderness;* make a straight highway for our God in the desert.*
Context
1Wafarijini, wafarijini watu wangu,
asema Mungu wenu. 2Sema na Yerusalemu kwa upole,
umtangazie
kwamba kazi yake ngumu imekamilika,
kwamba dhambi yake imefanyiwa fidia,
kwamba amepokea kutoka mkononi mwa Bwana
maradufu kwa ajili ya dhambi zake zote. 3Sauti ya mtu aliaye:
“Itengenezeni jangwani njia ya Bwana,
nyoosheni njia kuu nyikani
kwa ajili ya Mungu wetu. 4Kila bonde litainuliwa,
kila mlima na kilima kitashushwa;
penye mabonde patanyooshwa,
napo palipoparuza patasawazishwa. 5Utukufu wa Bwana utafunuliwa,
nao wanadamu wote watauona pamoja.
Kwa maana kinywa cha Bwana kimenena.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.