Isaya 40:16
Isaiah 40:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni, wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa.
Isaiah 40:16 in English
Isaiah 40:16 · Berean Standard Bible
Lebanon is not sufficient for fuel, nor its animals enough for a burnt offering.
Context
14Ni nani ambaye Bwana ametaka shauri kwake ili kumwelimisha,
naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?
Ni nani aliyemfundisha maarifa
au kumwonyesha mapito ya ufahamu? 15Hakika mataifa ni kama tone ndani ya ndoo,
ni kama vumbi jembamba juu ya mizani,
huvipima visiwa kana kwamba vilikuwa vumbi laini. 16Lebanoni hautoshi kwa moto wa madhabahuni,
wala wanyama wake hawatoshi kwa sadaka za kuteketezwa. 17Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu,
yanaonekana yasio na thamani
na zaidi ya bure kabisa. 18Basi, utamlinganisha Mungu na nani?
Utamlinganisha na kitu gani?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.