Isaya 4:2
Isaiah 4:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku ile Tawi la Bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika.
Isaiah 4:2 in English
Isaiah 4:2 · Berean Standard Bible
On that day the Branch of the LORD will be beautiful and glorious, and the fruit of the land will be the pride and glory of Israel’s survivors.
Context
1Katika siku ile wanawake saba
watamshika mwanaume mmoja
wakisema, “Tutakula chakula chetu wenyewe
na kuvaa nguo zetu wenyewe,
ila wewe uturuhusu tu tuitwe kwa jina lako.
Utuondolee aibu yetu!” 2Katika siku ile Tawi la Bwana litakuwa zuri na lenye utukufu, nalo tunda la nchi litakuwa fahari na utukufu wa wale Waisraeli watakaonusurika. 3Wale watakaoachwa Sayuni, watakaobaki Yerusalemu, wataitwa watakatifu, wale wote ambao wameorodheshwa miongoni mwa walio hai huko Yerusalemu. 4Bwana atausafisha uchafu wa wanawake wa Sayuni, atatakasa madoa ya damu kutoka Yerusalemu kwa Roho ya hukumu na Roho ya moto.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.