Isaya 37:35
Isaiah 37:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Nitaulinda mji huu na kuuokoa, kwa ajili yangu mwenyewe, na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu!”
Isaiah 37:35 in English
Isaiah 37:35 · Berean Standard Bible
‘I will defend this city and save it for My own sake and for the sake of My servant David.’”
Context
33“Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana kuhusu mfalme wa Ashuru:
“Hataingia katika mji huu
wala hatapiga mshale hapa.
Hatakuja mbele yake na ngao
wala kupanga majeshi kuuzingira. 34Kwa njia ile aliyoijia ndiyo atakayorudi;
hataingia katika mji huu,”
asema Bwana. 35“Nitaulinda mji huu na kuuokoa,
kwa ajili yangu mwenyewe,
na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu!” 36Ndipo malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi 185,000 katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali! 37Basi Senakeribu mfalme wa Ashuru akavunja kambi na kuondoka. Akarudi Ninawi na kukaa huko.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.