Native Bible

Isaiah 34:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Waliouawa watatupwa nje, maiti zao zitatoa uvundo, milima itatota kwa damu zao.

Isaiah 34:3 in English

Isaiah 34:3 · Berean Standard Bible

Their slain will be left unburied, and the stench of their corpses will rise; the mountains will flow with their blood.

Context

1Njooni karibu, enyi mataifa, nanyi msikilize; sikilizeni kwa makini, enyi kabila za watu! Dunia na isikie, navyo vyote vilivyo ndani yake, ulimwengu na vyote vitokavyo ndani yake! 2Bwana ameyakasirikia mataifa yote; ghadhabu yake ni juu ya majeshi yao yote. Atawaangamiza kabisa, atawatia mikononi mwa wachinjaji. 3Waliouawa watatupwa nje, maiti zao zitatoa uvundo, milima itatota kwa damu zao. 4Nyota zote za mbinguni zitayeyuka na anga litasokotwa kama kitabu, jeshi lote la angani litaanguka kama majani yaliyonyauka kutoka kwenye mzabibu, kama tini iliyonyauka kutoka kwenye mtini. 5Upanga wangu umekunywa na kushiba huko mbinguni, tazama, unashuka katika hukumu juu ya Edomu, wale watu ambao nimeshawahukumu, kuwaangamiza kabisa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.