Isaya 30:14
Isaiah 30:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo ukipasuka pasipo huruma ambapo katika vipande vyake hakuna kipande kitakachopatikana kwa kuukulia makaa kutoka jikoni au kuchotea maji kisimani.”
Isaiah 30:14 in English
Isaiah 30:14 · Berean Standard Bible
It will break in pieces like a potter’s jar, shattered so that no fragment can be found. Not a shard will be found in the dust large enough to scoop the coals from a hearth or to skim the water from a cistern.”
Context
12Kwa hiyo, hili ndilo asemalo yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli:
“Kwa sababu mmekataa ujumbe huu,
mkategemea uonevu na kutumainia udanganyifu, 13dhambi hii itakuwa kwenu
kama ukuta mrefu,
wenye ufa na wenye kubetuka,
ambao unaanguka ghafula,
mara moja. 14Utavunjika vipande vipande kama chombo cha udongo
ukipasuka pasipo huruma
ambapo katika vipande vyake
hakuna kipande kitakachopatikana
kwa kuukulia makaa kutoka jikoni
au kuchotea maji kisimani.” 15Hili ndilo Bwana Mwenyezi, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, asemalo:
“Katika kutubu na kupumzika ndio wokovu wenu,
katika kutulia na kutumaini ndizo nguvu zenu,
lakini hamkutaka. 16Mlisema, ‘Hapana, tutakimbia kwa farasi.’
Kwa hiyo mtakimbia!
Mlisema, ‘Tutakimbia kwa farasi waendao kasi.’
Kwa hiyo wanaowafukuza watakwenda kasi!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.