Isaya 29:5
Isaiah 29:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini adui zako wengi watakuwa kama vumbi laini, kundi la wakatili watakuwa kama makapi yapeperushwayo. Naam, ghafula, mara moja,
Isaiah 29:5 in English
Isaiah 29:5 · Berean Standard Bible
But your many foes will be like fine dust, the multitude of the ruthless like blowing chaff. Then suddenly, in an instant,
Context
3Nitapiga kambi pande zote dhidi yako,
nitakuzunguka kwa minara
na kupanga mazingirwa yangu dhidi yako. 4Utakaposhushwa, utanena kutoka ardhini,
utamumunya maneno yako kutoka mavumbini.
Sauti yako itatoka katika nchi kama vile ya mzimu,
utanongʼona maneno yako toka mavumbini. 5Lakini adui zako wengi watakuwa kama vumbi laini,
kundi la wakatili watakuwa
kama makapi yapeperushwayo.
Naam, ghafula, mara moja, 6Bwana Mwenye Nguvu Zote atakuja
na ngurumo, tetemeko la ardhi, na kwa sauti kuu,
atakuja na dhoruba, tufani na miali ya moto iteketezayo. 7Kisha makundi ya mataifa yote yale yapiganayo dhidi ya Arieli,
yale yanayomshambulia yeye na ngome zake, na kumzunguka kwa jeshi,
watakuwa kama ilivyo ndoto,
kama maono wakati wa usiku:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.