Isaya 29:21
Isaiah 29:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
wale ambao kwa neno humfanya mtu kuwa mwenye hatia, wamtegeao mtego mtetezi katika mahakama, na kwa ushuhuda wa uongo humnyima haki yeye asiye na hatia.
Isaiah 29:21 in English
Isaiah 29:21 · Berean Standard Bible
those who indict a man with a word, who ensnare the mediator at the gate, and who with false charges deprive the innocent of justice.
Context
19Mara nyingine tena wanyenyekevu watafurahi katika Bwana,
wahitaji watafurahi katika yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. 20Wakatili watatoweka na wenye kudhihaki watatokomea,
nao wote wenye jicho la uovu watakatiliwa mbali, 21wale ambao kwa neno humfanya mtu kuwa mwenye hatia,
wamtegeao mtego mtetezi katika mahakama,
na kwa ushuhuda wa uongo humnyima haki
yeye asiye na hatia. 22Kwa hiyo hili ndilo Bwana, aliyemkomboa Abrahamu, analosema kwa nyumba ya Yakobo:
“Yakobo hataaibishwa tena,
wala nyuso zao hazitabadilika sura tena. 23Wakati watakapoona watoto wao miongoni mwao,
kazi ya mikono yangu,
watalitakasa Jina langu takatifu;
wataukubali utakatifu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Yakobo,
nao watamcha Mungu wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.