Isaya 29:10
Isaiah 29:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana amewaleteeni usingizi mzito: Ameziba macho yenu (ninyi manabii); amefunika vichwa vyenu (ninyi waonaji).
Isaiah 29:10 in English
Isaiah 29:10 · Berean Standard Bible
For the LORD has poured out on you a spirit of deep sleep. He has shut your eyes, O prophets; He has covered your heads, O seers.
Context
8kama vile mtu aliye na njaa aotavyo kuwa anakula,
lakini huamka, bado njaa yake ingalipo,
kama vile mtu mwenye kiu aotavyo kuwa anakunywa maji,
lakini huamka akiwa anazimia, akiwa bado angali ana kiu.
Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa makundi yote ya mataifa
yanayopigana dhidi ya Mlima Sayuni. 9Duwaeni na kushangaa,
jifanyeni vipofu wenyewe na msione,
leweni, lakini si kwa mvinyo,
pepesukeni lakini si kwa kileo. 10Bwana amewaleteeni usingizi mzito:
Ameziba macho yenu (ninyi manabii);
amefunika vichwa vyenu (ninyi waonaji). 11Kwa maana kwenu ninyi, maono haya yote si kitu ila maneno yaliyotiwa lakiri katika kitabu. Kama mkimpa mtu yeyote awezaye kusoma kitabu hiki, nanyi mkamwambia, “Tafadhali kisome,” yeye atajibu, “Mimi siwezi, kwa kuwa kimetiwa lakiri.” 12Au kama mkimpa mtu yeyote kitabu hiki asiyeweza kusoma na kumwambia, “Tafadhali kisome,” atajibu, “Mimi sijui kusoma.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.