Isaya 28:26
Isaiah 28:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mungu wake humwelekeza na kumfundisha njia iliyo sahihi.
Isaiah 28:26 in English
Isaiah 28:26 · Berean Standard Bible
For his God instructs and teaches him properly.
Context
24Wakati mkulima alimapo ili apande,
je, hulima siku zote?
Je, huendelea kubomoa ardhi
na kusawazisha udongo? 25Akiisha kusawazisha shamba,
je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira?
Je, hapandi ngano katika sehemu yake,
shayiri katika eneo lake,
na nafaka nyingine katika shamba lake? 26Mungu wake humwelekeza
na kumfundisha njia iliyo sahihi. 27Iliki haipurwi kwa nyundo,
wala gurudumu la gari halivingirishwi juu ya jira;
iliki hupurwa kwa fimbo,
na jira kwa ufito. 28Nafaka lazima isagwe ili kutengeneza mkate,
kwa hiyo mtu haendelei kuipura daima.
Ingawa huendesha magurudumu ya gari lake la kupuria juu yake,
farasi wake hawasagi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.