Isaya 28:24
Isaiah 28:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wakati mkulima alimapo ili apande, je, hulima siku zote? Je, huendelea kubomoa ardhi na kusawazisha udongo?
Isaiah 28:24 in English
Isaiah 28:24 · Berean Standard Bible
Does the plowman plow for planting every day? Does he continuously loosen and harrow the soil?
Context
22Sasa acheni dharau zenu,
la sivyo minyororo yenu itakuwa mizito zaidi.
Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, ameniambia
habari za maangamizi yaliyoamriwa dhidi ya nchi yote. 23Sikilizeni msikie sauti yangu,
tegeni masikio na msikie niyasemayo. 24Wakati mkulima alimapo ili apande,
je, hulima siku zote?
Je, huendelea kubomoa ardhi
na kusawazisha udongo? 25Akiisha kusawazisha shamba,
je, hatapanyi mbegu za bizari na kutawanya jira?
Je, hapandi ngano katika sehemu yake,
shayiri katika eneo lake,
na nafaka nyingine katika shamba lake? 26Mungu wake humwelekeza
na kumfundisha njia iliyo sahihi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.