Isaya 28:11
Isaiah 28:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sawa kabisa, kwa midomo migeni na kwa lugha ngeni, Mungu atasema na watu hawa,
Isaiah 28:11 in English
Isaiah 28:11 · Berean Standard Bible
Indeed, with mocking lips and foreign tongues, He will speak to this people *
Context
9“Yeye anajaribu kumfundisha nani?
Yeye anamwelezea nani ujumbe wake?
Je, ni kwa watoto walioachishwa kunyonya?
Je, ni wale ambao ndipo tu wametolewa matitini? 10Kwa maana ni:
Amri juu ya amri, amri juu ya amri,
kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni;
hapa kidogo, kule kidogo.” 11Sawa kabisa, kwa midomo migeni
na kwa lugha ngeni,
Mungu atasema na watu hawa, 12wale ambao aliwaambia,
“Hapa ni mahali pa kupumzika,
waliochoka na wapumzike,”
na, “Hapa ni mahali pa mapumziko,”
lakini hawakutaka kusikiliza. 13Hivyo basi, neno la Bwana kwao litakuwa:
Amri juu ya amri, amri juu ya amri,
kanuni juu ya kanuni, kanuni juu ya kanuni,
hapa kidogo, kule kidogo:
ili waende na kuanguka chali,
wakijeruhiwa, wakinaswa na kukamatwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.