Isaya 26:21
Isaiah 26:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama, Bwana anakuja kutoka makao yake ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao. Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake, wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.
Isaiah 26:21 in English
Isaiah 26:21 · Berean Standard Bible
For behold, the LORD is coming out of His dwelling to punish the inhabitants of the earth for their iniquity. The earth will reveal her bloodshed and will no longer conceal her slain.
Context
19Lakini wafu wenu wataishi,
nayo miili yao itafufuka.
Ninyi mnaokaa katika mavumbi,
amkeni mkapige kelele kwa furaha.
Umande wenu ni kama umande wa asubuhi,
dunia itawazaa wafu wake. 20Nendeni, watu wangu, ingieni vyumbani mwenu
na mfunge milango nyuma yenu,
jificheni kwa kitambo kidogo
mpaka ghadhabu yake ipite. 21Tazama, Bwana anakuja kutoka makao yake
ili kuwaadhibu watu wa dunia kwa ajili ya dhambi zao.
Dunia itadhihirisha umwagaji damu juu yake,
wala haitaendelea kuwaficha watu wake waliouawa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.