Isaya 25:6
Isaiah 25:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Juu ya mlima huu Bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa karamu ya vinono kwa mataifa yote, karamu ya mvinyo wa zamani, nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana.
Isaiah 25:6 in English
Isaiah 25:6 · Berean Standard Bible
On this mountain the LORD of Hosts will prepare a banquet for all the peoples, a feast of aged wine, of choice meat, of finely aged wine.
Context
4Umekuwa kimbilio la watu maskini,
kimbilio la mhitaji katika taabu yake,
hifadhi wakati wa dhoruba
na kivuli wakati wa hari.
Kwa maana pumzi ya wakatili
ni kama dhoruba ipigayo ukuta 5na kama joto la jangwani.
Wewe wanyamazisha makelele ya wageni;
kama vile hari ipunguzwavyo na kivuli cha wingu,
ndivyo wimbo wa wakatili unyamazishwavyo. 6Juu ya mlima huu Bwana Mwenye Nguvu Zote ataandaa
karamu ya vinono kwa mataifa yote,
karamu ya mvinyo wa zamani,
nyama nzuri sana na divai zilizo bora sana. 7Juu ya mlima huu ataharibu
sitara ihifadhiyo mataifa yote,
kile kifuniko kifunikacho mataifa yote, 8yeye atameza mauti milele.
Bwana Mwenyezi atafuta machozi katika nyuso zote;
ataondoa aibu ya watu wake duniani kote.
Bwana amesema hili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.