Native Bible

Isaiah 23:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Habari ifikapo Misri, watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro.

Isaiah 23:5 in English

Isaiah 23:5 · Berean Standard Bible

When the report reaches Egypt, they will writhe in agony over the news of Tyre.

Context

3Kwenye maji makuu nafaka za Shihori zilikuja; mavuno ya Naili yalikuwa mapato ya Tiro, naye akawa soko la mataifa. 4Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari, kwa kuwa bahari imesema: “Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa, wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.” 5Habari ifikapo Misri, watakuwa katika maumivu makuu kwa ajili ya taarifa kutoka Tiro. 6Vukeni mpaka Tarshishi, ombolezeni, enyi watu wa kisiwani. 7Je, huu ndio mji wenu uliojaa sherehe, mji wa zamani, zamani kabisa ambao miguu yake imeuchukua kufanya makao nchi za mbali sana?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.