Isaya 23:2
Isaiah 23:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani, pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni, ambao mabaharia wamewatajirisha.
Isaiah 23:2 in English
Isaiah 23:2 · Berean Standard Bible
Be silent, O dwellers of the coastland, you merchants of Sidon, whose traders have crossed the sea.*
Context
1Neno kuhusu Tiro:
Ombolezeni, enyi meli za Tarshishi!
Kwa kuwa Tiro imeangamizwa,
imeachwa bila nyumba wala bandari.
Kuanzia nchi ya Kitimu*
neno limewajia. 2Nyamazeni kimya, enyi watu wa kisiwani,
pia ninyi wafanyabiashara wa Sidoni,
ambao mabaharia wamewatajirisha. 3Kwenye maji makuu
nafaka za Shihori zilikuja;
mavuno ya Naili yalikuwa mapato ya Tiro,
naye akawa soko la mataifa. 4Uaibishwe ee Sidoni, nawe ee ngome la bahari,
kwa kuwa bahari imesema:
“Sijapata kuwa na uchungu wa kuzaa wala sijapata kuzaa,
wala sijapata kulea wana wala kutunza mabinti.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.