Isaya 22:15
Isaiah 22:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asemalo: “Nenda ukamwambie huyu wakili Shebna, ambaye ni msimamizi wa jumba la kifalme:
Isaiah 22:15 in English
Isaiah 22:15 · Berean Standard Bible
This is what the Lord GOD of Hosts says: “Go, say to Shebna, the steward in charge of the palace:
Context
13Lakini tazama, kuna furaha na sherehe,
kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo,
kula nyama na kunywa mvinyo!
Mnasema, “Tuleni na kunywa,
kwa kuwa kesho tutakufa!” 14Bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.” 15Hili ndilo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote, asemalo:
“Nenda ukamwambie huyu wakili Shebna,
ambaye ni msimamizi wa jumba la kifalme: 16Unafanya nini hapa, na ni nani aliyekupa ruhusa
kujikatia kaburi lako mwenyewe,
ukichonga kaburi lako mahali palipo juu,
na kutoboa kwa patasi mahali pako pa kupumzikia katika mwamba? 17“Jihadhari, Bwana yu karibu kukukamata thabiti,
na kukutupa mbali, ewe mtu mwenye nguvu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.