Isaya 22:11
Isaiah 22:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani, lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza, au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale.
Isaiah 22:11 in English
Isaiah 22:11 · Berean Standard Bible
You built a reservoir between the walls for the waters of the ancient pool, but you did not look to the One who made it, or consider Him who planned it long ago.
Context
9mkaona kuwa Mji wa Daudi
una matundu mengi katika ulinzi wake,
mkaweka akiba ya maji
kwenye Bwawa la Chini. 10Mlihesabu majengo katika Yerusalemu
nanyi mkabomoa nyumba ili kuimarisha ukuta. 11Mlijenga bwawa la maji katikati ya kuta mbili
kwa ajili ya maji ya Bwawa la Zamani,
lakini hamkumtazama Yule aliyelitengeneza,
au kuwa na heshima kwa Yule aliyeubuni tangu zamani za kale. 12Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
aliwaita siku ile
ili kulia na kuomboleza,
kungʼoa nywele zenu na kuvaa nguo ya gunia. 13Lakini tazama, kuna furaha na sherehe,
kuchinja ngʼombe na kuchinja kondoo,
kula nyama na kunywa mvinyo!
Mnasema, “Tuleni na kunywa,
kwa kuwa kesho tutakufa!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.