Isaya 2:20
Isaiah 2:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Siku ile, watu watawatupia panya na popo sanamu zao za fedha na za dhahabu, walizozitengeneza ili waziabudu.
Isaiah 2:20 in English
Isaiah 2:20 · Berean Standard Bible
In that day men will cast away to the moles and bats their idols of silver and gold— the idols they made to worship.
Context
18nazo sanamu zitatoweka kabisa. 19Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba,
na kwenye mahandaki ardhini
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia. 20Siku ile, watu watawatupia
panya na popo
sanamu zao za fedha na za dhahabu,
walizozitengeneza ili waziabudu. 21Watakimbilia kwenye mapango miambani
na kwenye nyufa za miamba
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia. 22Acheni kumtumainia mwanadamu,
ambaye hana kitu ila pumzi katika pua zake.
Yeye ana thamani gani?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.