Isaya 2:19
Isaiah 2:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
Isaiah 2:19 in English
Isaiah 2:19 · Berean Standard Bible
Men will flee to caves in the rocks and holes in the ground, away from the terror of the LORD and from the splendor of His majesty, when He rises to shake the earth.
Context
17Majivuno ya mwanadamu yatashushwa,
na kiburi cha wanadamu kitanyenyekezwa,
Bwana peke yake ndiye atatukuzwa siku hiyo, 18nazo sanamu zitatoweka kabisa. 19Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba,
na kwenye mahandaki ardhini
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia. 20Siku ile, watu watawatupia
panya na popo
sanamu zao za fedha na za dhahabu,
walizozitengeneza ili waziabudu. 21Watakimbilia kwenye mapango miambani
na kwenye nyufa za miamba
kutokana na utisho wa Bwana
na utukufu wa enzi yake,
ainukapo kuitikisa dunia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.