Isaya 16:7
Isaiah 16:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo Wamoabu wanaomboleza, wanaiombolezea Moabu kwa pamoja. Wanaomboleza na kuhuzunika kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi.
Isaiah 16:7 in English
Isaiah 16:7 · Berean Standard Bible
Therefore let Moab wail; let them wail together for Moab. Moan for the raisin cakes of Kir-hareseth, you who are utterly stricken.
Context
5Kwa upendo kiti cha enzi kitaimarishwa,
kwa uaminifu mtu ataketi juu yake,
yeye atokaye nyumba ya Daudi:
yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki,
na huhimiza njia ya haki. 6Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu:
kiburi chake cha kujivuna na udanganyifu,
kiburi chake na ufidhuli wake,
lakini majivuno yake si kitu. 7Kwa hiyo Wamoabu wanaomboleza,
wanaiombolezea Moabu kwa pamoja.
Wanaomboleza na kuhuzunika
kwa ajili ya watu wa Kir-Haresethi. 8Mashamba ya Heshboni yananyauka,
pia na mizabibu ya Sibma.
Watawala wa mataifa
wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana,
ambayo ilipata kufika Yazeri
na kuenea kuelekea jangwani.
Machipukizi yake yalienea
yakafika hadi baharini. 9Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo,
kwa ajili ya mizabibu ya Sibma.
Ee Heshboni, ee Eleale,
ninakulowesha kwa machozi!
Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva
na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.