Isaya 15:3
Isaiah 15:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wamevaa nguo za magunia barabarani, juu ya mapaa na kwenye viwanja wote wanaomboleza, wamelala kifudifudi kwa kulia.
Isaiah 15:3 in English
Isaiah 15:3 · Berean Standard Bible
In its streets they wear sackcloth; on the rooftops and in the public squares they all wail, falling down weeping.
Context
1Neno kuhusu Moabu:
Ari iliyo Moabu imeangamizwa:
imeharibiwa kwa usiku mmoja!
Kiri iliyo Moabu imeangamizwa,
imeharibiwa kwa usiku mmoja! 2Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake,
mpaka mahali pake pa juu ili walie,
Moabu anaombolezea Nebo na Medeba.
Kila kichwa kimenyolewa
na kila ndevu limeondolewa. 3Wamevaa nguo za magunia barabarani,
juu ya mapaa na kwenye viwanja
wote wanaomboleza,
wamelala kifudifudi kwa kulia. 4Heshboni na Eleale wanalia,
sauti zao zinasikika hadi Yahazi.
Kwa hiyo watu wenye silaha wa Moabu wanapiga kelele,
nayo mioyo yao imezimia. 5Moyo wangu unamlilia Moabu;
wakimbizi wake wanakimbilia Soari,
hadi Eglath-Shelishiya.
Wanapanda njia ya kwenda Luhithi,
wanakwenda huku wanalia;
barabarani iendayo Horonaimu
wanaombolezea maangamizi yao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.