Isaya 13:19
Isaiah 13:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Babeli, johari ya falme, utukufu wa kiburi cha Wababeli,* itaangushwa na Mungu kama Sodoma na Gomora.
Isaiah 13:19 in English
Isaiah 13:19 · Berean Standard Bible
And Babylon, the jewel of the kingdoms, the glory of the pride of the Chaldeans, will be overthrown by God like Sodom and Gomorrah.
Context
17Tazama, nitawachochea Wamedi dhidi yao,
ambao hawajali fedha
wala hawafurahii dhahabu. 18Mishale yao itawaangusha vijana,
hawatakuwa na huruma kwa watoto wachanga
wala hawataangalia watoto kwa huruma. 19Babeli, johari ya falme,
utukufu wa kiburi cha Wababeli,*
itaangushwa na Mungu
kama Sodoma na Gomora. 20Hautakaliwa na watu kamwe
wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote.
Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko,
hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake huko. 21Lakini viumbe wa jangwani watalala huko,
mbweha watajaza nyumba zake,
bundi wataishi humo
nao mbuzi-mwitu watarukaruka humo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.