Isaya 10:18
Isaiah 10:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Fahari ya misitu yake na mashamba yenye rutuba utateketeza kabisa, kama vile mtu mgonjwa adhoofikavyo.
Isaiah 10:18 in English
Isaiah 10:18 · Berean Standard Bible
The splendor of its forests and orchards, both soul and body, it will completely destroy, as a sickness consumes a man.
Context
16Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
atatuma ugonjwa wa kudhoofisha kwa askari wake walio hodari,
katika fahari yake moto utawaka
kama mwali wa moto. 17Nuru ya Israeli itakuwa moto,
Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto;
katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba
na michongoma yake. 18Fahari ya misitu yake na mashamba yenye rutuba
utateketeza kabisa,
kama vile mtu mgonjwa adhoofikavyo. 19Nayo miti inayobaki katika misitu yake itakuwa michache sana
hata mtoto mdogo angeweza kuihesabu. 20Katika siku ile, mabaki ya Israeli,
walionusurika wa nyumba ya Yakobo,
hawatamtegemea tena yeye aliyewapiga,
lakini watamtegemea kwa kweli
Bwana Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.