Isaya 1:25
Isaiah 1:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu, nitawasafisha takataka zenu zote na kuwaondolea unajisi wenu wote.
Isaiah 1:25 in English
Isaiah 1:25 · Berean Standard Bible
I will turn My hand against you; I will thoroughly purge your dross; I will remove all your impurities.
Context
23Watawala wenu ni waasi,
rafiki wa wevi,
wote wanapenda rushwa
na kukimbilia hongo.
Hawatetei yatima,
shauri la mjane haliletwi mbele yao lisikilizwe. 24Kwa hiyo Bwana, Bwana Mwenye Nguvu Zote,
Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi:
“Lo, nitapata faraja kutoka kwa adui zangu
na kujilipizia kisasi juu ya watesi wangu. 25Nitauelekeza mkono wangu dhidi yenu,
nitawasafisha takataka zenu zote
na kuwaondolea unajisi wenu wote. 26Nitawarudishia waamuzi wenu kama ilivyokuwa siku za zamani,
nao washauri wenu kama ilivyokuwa mwanzoni.
Baadaye utaitwa,
Mji wa Haki,
Mji Mwaminifu.” 27Sayuni itakombolewa kwa haki,
wale waliomo ndani yake waliotubu kwa uaminifu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.