Isaya 1:20
Isaiah 1:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
lakini kama mkikataa na kuasi, mtaangamizwa kwa upanga.” Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena.
Isaiah 1:20 in English
Isaiah 1:20 · Berean Standard Bible
But if you resist and rebel, you will be devoured by the sword.” For the mouth of the LORD has spoken.
Context
18“Njooni basi tuhojiane,”
asema Bwana.
“Ingawa dhambi zenu ni kama rangi nyekundu,
zitakuwa nyeupe kama theluji;
ingawa ni nyekundu sana kama damu,
zitakuwa nyeupe kama sufu. 19Kama mkikubali na kutii,
mtakula mema ya nchi, 20lakini kama mkikataa na kuasi,
mtaangamizwa kwa upanga.”
Kwa kuwa kinywa cha Bwana kimenena. 21Tazama jinsi mji uliokuwa mwaminifu
umekuwa kahaba!
Mwanzoni ulikuwa umejaa unyofu,
haki ilikuwa inakaa ndani yake,
lakini sasa ni wauaji! 22Fedha yenu imekuwa takataka,
divai yenu nzuri imechanganywa na maji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.