Hosea 9:16
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Efraimu ameharibiwa, mzizi wao umenyauka, hawazai tunda. Hata kama watazaa watoto, nitawachinja watoto wao waliotunzwa vizuri.”
Hosea 9:16 in English
Hosea 9:16 · Berean Standard Bible
Ephraim is struck down; their root is withered; they cannot bear fruit. Even if they bear children, I will slay the darlings of their wombs.
Context
14Wape, Ee Bwana,
je, utawapa nini?
Wape matumbo ya kuharibu mimba
na matiti yaliyokauka. 15“Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali,
niliwachukia huko.
Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi,
nitawafukuza katika nyumba yangu.
Sitawapenda tena,
viongozi wao wote ni waasi. 16Efraimu ameharibiwa,
mzizi wao umenyauka,
hawazai tunda.
Hata kama watazaa watoto,
nitawachinja watoto wao
waliotunzwa vizuri.” 17Mungu wangu atawakataa
kwa sababu hawakumtii;
watakuwa watu wa kutangatanga
miongoni mwa mataifa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.