Hosea 8:6
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Zimetoka katika Israeli! Ndama huyu: ametengenezwa na fundi, si Mungu. Atavunjwa vipande vipande, yule ndama wa Samaria.
Hosea 8:6 in English
Hosea 8:6 · Berean Standard Bible
For this thing is from Israel— a craftsman made it, and it is not God. It will be broken to pieces, that calf of Samaria.
Context
4Wanaweka wafalme bila idhini yangu,
wamechagua wakuu bila kibali changu.
Kwa fedha zao na dhahabu
wamejitengenezea sanamu kwa ajili
ya maangamizi yao wenyewe. 5Ee Samaria, tupilieni mbali sanamu yenu ya ndama!
Hasira yangu inawaka dhidi yao.
Watakuwa najisi mpaka lini? 6Zimetoka katika Israeli!
Ndama huyu: ametengenezwa na fundi, si Mungu.
Atavunjwa vipande vipande,
yule ndama wa Samaria. 7“Wanapanda upepo
na kuvuna upepo wa kisulisuli.
Bua halina suke,
halitatoa unga.
Kama lingetoa nafaka,
wageni wangeila yote. 8Israeli amemezwa;
sasa yupo miongoni mwa mataifa
kama kitu kisicho na thamani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.