Hosea 4:16
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Waisraeli ni wakaidi, kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi. Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga kama wana-kondoo katika shamba la majani?
Hosea 4:16 in English
Hosea 4:16 · Berean Standard Bible
For Israel is as obstinate as a stubborn heifer. Can the LORD now shepherd them like lambs in an open meadow?
Context
14“Sitawaadhibu binti zenu wakati
wanapogeukia ukahaba,
wala wake za wana wenu
wanapofanya uzinzi,
kwa sababu wanaume wenyewe huandamana na malaya
na kutambikia pamoja na makahaba
wa mahali pa kuabudia miungu:
watu wasiokuwa na ufahamu
wataangamia! 15“Ingawa umefanya uzinzi, ee Israeli,
Yuda naye asije akawa na hatia.
“Usiende Gilgali,
usipande kwenda Beth-Aveni*
Wala usiape,
‘Hakika kama Bwana aishivyo!’ 16Waisraeli ni wakaidi,
kama mtamba wa ngʼombe ambaye ni mkaidi.
Ni jinsi gani basi Bwana anaweza kuwachunga
kama wana-kondoo
katika shamba la majani? 17Efraimu amejiunga na sanamu,
ondokana naye! 18Hata wakati wamemaliza vileo vyao
wanaendelea na ukahaba wao,
watawala wao hupenda sana
njia za aibu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.