Hosea 2:4
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sitaonyesha upendo wangu kwa watoto wake, kwa sababu ni watoto wa uzinzi.
Hosea 2:4 in English
Hosea 2:4 · Berean Standard Bible
I will have no compassion on her children, because they are the children of adultery.
Context
2“Mkemeeni mama yenu, mkemeeni,
kwa maana yeye si mke wangu,
nami si mume wake.
Aondoe sura ya uzinzi katika uso wake
na uzinzi kati ya matiti yake. 3Kama sivyo nitamvua nguo zake awe uchi
na kumwacha uchi kama siku ile aliyozaliwa.
Nitamfanya kama jangwa,
nitamgeuza awe nchi ya kiu,
nami nitamuua kwa kiu. 4Sitaonyesha upendo wangu kwa watoto wake,
kwa sababu ni watoto wa uzinzi. 5Mama yao amekosa uaminifu
na amewachukua mimba katika aibu.
Gomeri alisema, ‘Nitawaendea wapenzi wangu,
ambao hunipa chakula changu
na maji yangu,
sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu
na kinywaji changu.’ 6Kwa hiyo mimi Mungu nitaizuia njia yake
kwa vichaka vya miiba,
nitamjengea ukuta ili kwamba
asiweze kutoka.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.