Hosea 13:13
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Utungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia, lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima; wakati utakapowadia hatatoka katika tumbo la mama yake.
Hosea 13:13 in English
Hosea 13:13 · Berean Standard Bible
Labor pains come upon him, but he is an unwise son. When the time arrives, he fails to present himself at the opening of the womb.
Context
11Hivyo katika hasira yangu nilikupa mfalme
na katika ghadhabu yangu nilimwondoa. 12Kosa la Efraimu limehifadhiwa,
dhambi zake zimewekwa katika kumbukumbu. 13Utungu kama wa mwanamke anayejifungua mtoto humjia,
lakini yeye ni mtoto asiyekuwa na hekima;
wakati utakapowadia hatatoka
katika tumbo la mama yake. 14“Nitawakomboa watu hawa kutoka nguvu za kaburi,
nitawakomboa kutoka mautini.
Yako wapi, ee mauti, mateso yako?
Uko wapi, ee kuzimu, uharibifu wako?
“Sitakuwa na huruma, 15hata ingawa Efraimu atastawi
miongoni mwa ndugu zake.
Upepo wa mashariki kutoka kwa Bwana utakuja,
ukivuma kutoka jangwani,
chemchemi yake haitatoa maji
na kisima chake kitakauka.
Ghala lake litatekwa
hazina zake zote.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.