Hosea 12:2
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda, atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.
Hosea 12:2 in English
Hosea 12:2 · Berean Standard Bible
The LORD also brings a charge against Judah. He will punish Jacob * according to his ways and repay him according to his deeds.
Context
1Efraimu anajilisha upepo;
hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima
na kuzidisha uongo na jeuri.
Anafanya mkataba na Ashuru
na kutuma mafuta ya zeituni Misri. 2Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda,
atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake
na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake. 3Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake;
kama mwanadamu, alishindana na Mungu. 4Alishindana na malaika na kumshinda;
alilia na kuomba upendeleo wake.
Alimkuta huko Betheli
na kuzungumza naye huko:
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.