Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu, kwa vifungo vya upendo; niliondoa nira shingoni mwao nami nikainama kuwalisha.

Hosea 11:4 in English

Hosea 11:4 · Berean Standard Bible

I led them with cords of kindness, with ropes of love; I lifted the yoke from their necks and bent down to feed them.

Context

2Lakini kadiri nilivyomwita Israeli, ndivyo walivyokwenda mbali nami. Walitoa dhabihu kwa Mabaali na kufukiza uvumba kwa vinyago. 3Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea, nikiwashika mikono; lakini hawakutambua kuwa ni mimi niliyewaponya. 4Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu, kwa vifungo vya upendo; niliondoa nira shingoni mwao nami nikainama kuwalisha. 5“Je, hawatarudi Misri, nayo Ashuru haitawatawala kwa sababu wamekataa kutubu? 6Panga zitametameta katika miji yao, zitaharibu makomeo ya malango yao na kukomesha mipango yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.