Waebrania 7:22
Hebrews 7:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Hebrews 7:22 in English
Hebrews 7:22 · Berean Standard Bible
Because of this oath, Jesus has become the guarantee of a better covenant.
Context
20Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, 21lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia:
“Bwana ameapa
naye hatabadilisha mawazo yake:
‘Wewe ni kuhani milele.’ ” 22Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi. 23Basi pamekuwepo na makuhani wengi wa aina hiyo, kwa kuwa kifo kiliwazuia kuendelea na huduma yao ya ukuhani. 24Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, anao ukuhani wa kudumu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.