Waebrania 7:20
Hebrews 7:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote,
Hebrews 7:20 in English
Hebrews 7:20 · Berean Standard Bible
And none of this happened without an oath. For others became priests without an oath,
Context
18Kwa upande mmoja, ile amri ya mwanzo isiyofaa na dhaifu imebatilishwa 19(kwa maana sheria haikufanya kitu chochote kuwa kikamilifu). Kwa upande mwingine, tumeletewa tumaini lililo bora zaidi ambalo linatuleta karibu na Mungu. 20Nalo tumaini hilo halikutolewa pasipo kiapo! Wengine walikuwa makuhani pasipo kiapo chochote, 21lakini Yesu alifanywa kuhani kwa kiapo wakati Mungu alimwambia:
“Bwana ameapa
naye hatabadilisha mawazo yake:
‘Wewe ni kuhani milele.’ ” 22Kwa ajili ya kiapo hiki, Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo bora zaidi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.