Waebrania 4:8
Hebrews 4:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa maana kama Yoshua alikuwa amewapa raha, Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine.
Hebrews 4:8 in English
Hebrews 4:8 · Berean Standard Bible
For if Joshua had given them rest, God would not have spoken later about another day.
Context
6Kwa hiyo inabaki kuwa wazi kwa wengine kuingia, nao wale wa kwanza waliopokea Injili walishindwa kuingia kwa sababu ya kutokutii. 7Kwa hiyo Mungu ameweka siku nyingine, akaiita Leo, akisema kwa kinywa cha Daudi baadaye sana, kwa maneno yaliyotangulia kunenwa:
“Leo, kama mkiisikia sauti yake,
msiifanye mioyo yenu migumu.” 8Kwa maana kama Yoshua alikuwa amewapa raha, Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine. 9Kwa hiyo basi, imebaki raha ya Sabato kwa ajili ya watu wa Mungu; 10kwa kuwa kila mmoja aingiaye katika raha ya Mungu pia hupumzika kutoka kazi zake mwenyewe, kama vile Mungu alivyopumzika kutoka kazi zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.