Waebrania 4:3
Hebrews 4:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sasa sisi ambao tumeamini tunaingia katika ile raha, kama vile Mungu alivyosema, “Kwa hiyo nikaapa katika hasira yangu, ‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’ ” Lakini kazi yake ilikamilika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Hebrews 4:3 in English
Hebrews 4:3 · Berean Standard Bible
Now we who have believed enter that rest. As for the others, it is just as God has said: “So I swore on oath in My anger, ‘They shall never enter My rest.’”* And yet His works have been finished since the foundation of the world.
Context
1Kwa hiyo, kwa kuwa bado ahadi ya kuingia rahani iko wazi, tujihadhari ili hata mmoja wenu asije akaikosa. 2Kwa maana sisi pia tumesikia Injili iliyohubiriwa kwetu, kama nao walivyosikia; lakini ujumbe ule waliousikia haukuwa na maana kwao, kwa sababu wale waliousikia hawakuuchanganya na imani. 3Sasa sisi ambao tumeamini tunaingia katika ile raha, kama vile Mungu alivyosema,
“Kwa hiyo nikaapa katika hasira yangu,
‘Kamwe hawataingia rahani mwangu.’ ”
Lakini kazi yake ilikamilika tangu kuumbwa kwa ulimwengu. 4Kwa maana mahali fulani amezungumza kuhusu siku ya saba, akisema: “Katika siku ya saba Mungu alipumzika kutoka kazi zake zote.” 5Tena hapo juu asema, “Kamwe hawataingia rahani mwangu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.