Native Bible

Hebrews 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Pia Mungu aliushuhudia kwa ishara, maajabu na kwa miujiza mbalimbali, na karama za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake.

Hebrews 2:4 in English

Hebrews 2:4 · Berean Standard Bible

and was affirmed by God through signs, wonders, various miracles, and gifts of the Holy Spirit distributed according to His will.

Context

2Kwa kuwa kama ujumbe ulionenwa na malaika ulikuwa imara, na kila uasi na kutokutii kulipata adhabu ya haki, 3je, sisi tutapaje kupona kama tusipojali wokovu mkuu namna hii? Wokovu huu, ambao mwanzo ulitangazwa na Bwana, ulithibitishwa kwetu na wale waliomsikia. 4Pia Mungu aliushuhudia kwa ishara, maajabu na kwa miujiza mbalimbali, na karama za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake. 5Mungu hakuuweka ulimwengu ujao ambao tunanena habari zake chini ya malaika. 6Lakini kuna mahali mtu fulani ameshuhudia akisema: “Mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria, binadamu ni nani hata unamjali?

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.