Waebrania 10:23
Hebrews 10:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumbayumba, kwa maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.
Hebrews 10:23 in English
Hebrews 10:23 · Berean Standard Bible
Let us hold resolutely to the hope we profess, for He who promised is faithful.
Context
21basi kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu juu ya nyumba ya Mungu, 22sisi na tumkaribie Mungu kwa moyo mnyofu kwa imani timilifu, mioyo yetu ikiwa imenyunyizwa damu ya Kristo na kuwa safi kutokana na dhamiri mbaya nayo miili yetu ikiwa imeoshwa kwa maji safi. 23Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumbayumba, kwa maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu. 24Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema. 25Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi, bali tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.