Native Bible

Haggai 2:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi.

Haggai 2:21 in English

Haggai 2:21 · Berean Standard Bible

“Tell Zerubbabel governor of Judah that I am about to shake the heavens and the earth:

Context

19Je, bado kuna mbegu iliyobakia ghalani? Mpaka sasa, hakuna mzabibu au mtini, mkomamanga wala mzeituni uliozaa tunda. “ ‘Kuanzia leo na kuendelea, nitawabariki.’ ” 20Neno la Bwana likamjia Hagai kwa mara ya pili katika siku ya ishirini na nne ya mwezi kusema: 21“Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi. 22Nitapindua viti vya enzi vya falme, na kuziharibu kabisa nguvu za falme za kigeni. Nitapindua magari ya vita pamoja na waendeshaji wake; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa upanga wa ndugu yake. 23“ ‘Katika siku ile,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote, ‘nitakuchukua wewe, mtumishi wangu Zerubabeli mwana wa Shealtieli,’ asema Bwana. ‘Nitakufanya kama pete yangu ya muhuri, kwa kuwa nimekuchagua,’ asema Bwana Mwenye Nguvu Zote.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.