Hagai 2:20
Haggai 2:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Neno la Bwana likamjia Hagai kwa mara ya pili katika siku ya ishirini na nne ya mwezi kusema:
Haggai 2:20 in English
Haggai 2:20 · Berean Standard Bible
For the second time that day, the twenty-fourth day of the month, the word of the LORD came to Haggai, saying,
Context
18‘Tangu leo na kuendelea, kuanzia siku hii ya ishirini na nne ya mwezi wa tisa, tafakarini siku ambayo msingi wa Hekalu la Bwana uliwekwa. Tafakarini: 19Je, bado kuna mbegu iliyobakia ghalani? Mpaka sasa, hakuna mzabibu au mtini, mkomamanga wala mzeituni uliozaa tunda.
“ ‘Kuanzia leo na kuendelea, nitawabariki.’ ” 20Neno la Bwana likamjia Hagai kwa mara ya pili katika siku ya ishirini na nne ya mwezi kusema: 21“Mwambie Zerubabeli mtawala wa Yuda kwamba nitazitikisa mbingu na nchi. 22Nitapindua viti vya enzi vya falme, na kuziharibu kabisa nguvu za falme za kigeni. Nitapindua magari ya vita pamoja na waendeshaji wake; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa upanga wa ndugu yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.