Native Bible

Habakkuk 3:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

hata hivyo nitashangilia katika Bwana, nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.

Habakkuk 3:18 in English

Habakkuk 3:18 · Berean Standard Bible

yet I will exult in the LORD; I will rejoice in the God of my salvation!

Context

16Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu, midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti; uchakavu ukanyemelea mifupa yangu, na miguu yangu ikatetemeka. Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa kuyajilia mataifa yaliyotuvamia. 17Ingawa mtini hauchanui maua na hakuna zabibu juu ya mizabibu, ingawaje mzeituni hauzai, na hata mashamba hayatoi chakula, iwapo hakuna kondoo katika banda, wala ngʼombe katika zizi, 18hata hivyo nitashangilia katika Bwana, nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu. 19Bwana Mwenyezi ni nguvu yangu; huifanya miguu yangu kama miguu ya ayala, huniwezesha kupita juu ya vilima. Kwa kiongozi wa uimbaji. Kwa vinanda vyangu vya nyuzi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.